Thursday, 25 January 2018

Wananchi katika halmashauri ya Manispaa Mpanda mkoa katavi wamelitaka jeshi la polisi kutoa elimu juu ya alama za barabarani ili kupunguza ajali .


MPANDA

Wananchi katika halmashauri ya Manispaa Mpanda mkoa katavi wamelitaka jeshi la polisi kutoa elimu juu ya alama za barabarani ili kupunguza ajali .

Wakizungumza na mpanda radio kwa nyakati tofauti watumiaji wa barabara wamesema elimu ya usalama barabarani itawasaidia watembea kwa miguu kujiepusha na ajali za mara kwa mara zinazotokea kwa kutokujua matumizi ya alama hizo.

Kamanda wa usalama barabarani mkoa katavi John Mfinanga amesema kuwa elimu ya usalama barabarani na matumizi ya alama wanazitoa kupitia radio na katika vijiwe vya bodaboda ili kuwasaidia watembea kwa miguu kuweza kuzifahamu sheria na alama hizo.

Mfinanga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi pindi semina hizona kusema kwamba semina hizo zinatolewa bure na hazina malipo.

Chanzo: Furaha Kimondo 
#Changia Damu Okoa Taifa


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...