Picha ya wanafunzi wa shule ya sekondari Rungwa |
MPANDA
Takribani
wanafunzi 20 kutoka shule ya sekondari Rungwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi
wametembelea kituo cha Mpanda Redio
kujifunza masuala ya Tehama.
Wanafunzi
hao wamebainisha kupata uelewa kuhusu
Tehama na namna watakavyowafundisha wenzao namna kituo hiki kinavyotoa habari
kwa jamii pamoja na uandaaji wa
vipindi .
Picha ya wanafunzi wa shule ya sekondari Rungwa |
Kwa
upande wa Mwalimu wa Shule hiyo Gwamaka Mwaipisi ameshauri walimu wengine
kuwafundisha wanafunzi wao masuala ya tehema kutokana na kukua kwa teknolojia inayowataka wanafunzi kuelewa matumizi ya
komputa.
Meneja
wa kituo cha Mpanda Redio Revocatus Msafiri amewataka wananchi kutumia kituo hiki ipasavyo kwani iko kwajili ya wananchi wa
mkoa wa katavi .
Meneja wa Mpanda Fm bwana Revocatus Msafiri na Muhariri wetu Alinanuswe Edward wakiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Rungwa. |
No comments:
Post a Comment