Friday, 9 March 2018

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO AMELAANI KITENDO CHA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA ITENKA KUANDAA NJAMA ZA KUVURUGA MKUTANO MAAZIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE.


NSIMBO

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoa wa Katavi Raphael Karinga amelaani kitendo cha mwenyekiti wa kijiji cha Itenka Maiko Katambi kuandaa njama za kuvuruga mkutano wa maazimisho ya siku ya wanawake.

Karinga amezungumza kwa njia ya simu na kueleza kuwa  mwenyekiti huyo ambaye awali alikaimisha nafasi yake kwa mjumbe wa halmashauri ya Kijiji na kuibuka mwishoni mwa mkutano huku akitoa maneno ya kejeli kwa mkuu wawilaya ya Mpanda Liliani Matinga ni jambo lisilo kubalika.

Karinga amewaasa viongozi wa vijiji kujua namna ya kutatua changamoto mbali mbali wanazo kumbana nazo kuliko kukwamisha jitihada za serikali kwa makusudi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi Damasi Nyanda asubuhi ya leo ameongea kwa njia ya Simu na kufafanua kuwa hana taarifa ya kutiwa nguvuni kwa mwenyekiti huyo kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda.

 Chanzo: Ester Baraka

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...