Mstahiki Meya wa Manispaa Mpanda Mh.Willium Mbogo |
MPANDA
Baraza la Madiwani Halamshauri ya
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,limesema litachukua hatua kali za kisheria
ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi wa idara ya ardhi watakaosababisha migogoro
ya ardhi baina ya wananchi.
Tamko hilo ambalo limtolewa na
Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Willium Mbogo kupitia kikao maalumu cha
bajeti cha baraza hilo ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Aidha amesema hatua za kisheria zitachukuliwa
pia kwa watumishi wa idara mbalimbali ambao wamesababisha Manispaa ya Mpanda
Kukosa mapato kutokana na uzembe wao katika uwajibikaji.
Katika Kikao hicho cha siku
mbili,mambo mbalimbali yamejadiliwa katika rasmu ya bajeti ya mwaka wa fedha
2018,2019 ikiwemo masuala ya elimu,afya,miundombinu ya barabara pamoja na
ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.
Chanzo:Mpanda radio
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment