Thursday, 25 January 2018

Wananchi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuwa makini wanapofanya miamala yoyote ya pesa kwa watu wasiowafahamu vizuri ili kutokomeza utapeli wa pesa kimtandao ambao umeshamiri Mkoani Katavi.

KATAVI

Wananchi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuwa makini wanapofanya miamala yoyote ya pesa kwa watu wasiowafahamu vizuri ili kutokomeza utapeli wa pesa kimtandao ambao umeshamiri Mkoani Katavi.

Wito huo umetolewa na Afisa wa Polisi kutoka Ofisi ya Upelelezi Wilayani Mpanda Thobias Lindege ambapo ametoa elimu ya kupambana na uharifu wa kimtandao kupitia baraza maalumu la madiwani la Manispaa ya Mpanda.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo amesema wanatarajia kufuatilia  matangazo yanayobandikwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda yakiwemo yanayohusisha waganga wa jadi lengo likiwa ni kutokomeza utapeli.

Utapeli wa kimtandao kwa kiasi kikubwa umeikumba mifumo ya kibenki pamoja na simu za mikononi.

Chanzo:Mwananchi

#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...