UMOJA
WA MATAIFA
Ujumbe wa Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa utakwenda Washington Jumatatu ijayo, kuchunguza mabaki
ynayotokana na makombora yanayodaiwa yalitolewa na Iran kwa waasi wa Kihouthi
nchini Yemen.
Maafisa wa kibalozi wamesema
baadaye ujumbe huo wa Baraza la Usalama utakutana na maafisa wa Ikulu ya White
House.
Unatarajiwa kuonana na Rais
Donald Trump wa Marekani, wakati utawala wake ukitafuta uungaji mkono wa
Kimataifa dhidi ya Iran.
mwezi uliopita, balozi wa Marekani
katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, aliwasilisha mabaki hayo kama ushahidi
kwamba kombora lililofyatuliwa na waasi wa Houthi nchini Yemen dhidi ya Saudi
Arabia mwezi Novemba, lilitengenezwa Iran.
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment