Saturday, 18 November 2017

Fedha na mgawanyiko vyakwamisha COP23.


BERLIN

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaojulikana kama COP23,umekamilika rasmi jana usiku mjini Bonn Ujerumani.

Waziri Mkuu wa Fiji,Frank Bainimarama amesema wamepiga hatua nzuri kuhusu mkataba wa Paris ingawa mjumbe mkuu wa China,Xie Zhenhua amesema kuna masuala mengi ambayo bado yanapaswa kujadiliwa. Wajumbe wamesema mazungumzo yamekwama hasa katika masuala ya fedha na kuibuka tena mgawanyiko kati ya mataifa tajiri na yale yanayoendelea hasa inapohitajika kila upande kufanya juhudi katika kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi.

Nchi maskini duniani zimesema zinahitaji fedha ili kujiimarisha zaidi katika kujiandaa na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi huku Ujerumani ikisema  inalenga kupunguza matumizi ya gesi inayochafua mazingira kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020.

Desemba 12 mwaka huu,Rais wa Ufaransa,Emmanuel Macron amewaalika zaidi ya viongozi 100 mjini Paris kuadhimisha miaka miwili tangu ulipofikiwa mkataba wa Paris.

Source Dw swahil

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...