Rais wa zimbabwe Robert Mugabe |
HARARE
Chama tawala
nchini Zimbabwe ZANU-PF kimemtaka Rais Robert Mugabe ajiuzulu.
Matawi ya
chama hicho katika majimbo yote 10 yamekutana jana na ya memtaka Mugabe na
mkewe Grace ambaye azma yake ya kutaka kurithi madaraka kutoka kwa mumewe
imechochea mzozo wa kisiasa,kujiuzulu kutoka kwenye chama hicho.
Viongozi wa
chama hicho wamesema watamshinikiza kiongozi huyo kuondolewa katika uongozi wa
chama ifikapo kesho na kisha bunge litapiga kura ya kutokuwa na imani naye.
ZANU-PF leo
kimeitisha maandamano kuliunga mkono jeshi kwa kuchukua madaraka na
kumshinikiza Mugabe ajiuzulu na kesho kikitarajia kutafanya mkutano maalamu wa
kamati kuu kujadili yanayojiri kisiasa nchini humo. Waziri wa mambo ya nje wa
Marekani Rex Tillerson amewaambia mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika
wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano mjini Washington kuwa anahimiza kurejea haraka
kwa utawala wa kiraia Zimbabwe.
Wakati huo
huo,China imesema inatumai kuwa hali ya kisiasa inayoendelea Zimbabwe
itasuluhishwa kulingana na sheria na utulivu uterejea nchini humo.
Source Dw swahil
No comments:
Post a Comment