ZANZIBAR
WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini makubaliano
ya ushirikiano na Bohari ya Dawa Tanzania (msd) katika masuala ya uagiziaji
dawa na vifaa Tiba kutoka viwandani moja kwa moja ikiwa ni hatua itaiwezesha
Zanzibar kupunguza gharama kubwa ya kuagiza dawa kutoka katika makampuni.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Bi.Asha Abdalla Juma ametia saini kwa upande wa Wizara hiyo
huku Mkurugenzi Mkuu Laurean Rugambwa Bwanakunu akiiwakilisha
Bohari kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya
Zanzibari Mnazimmoja.
Akizungumza
baada ya kutiliana sani Bi.Asha Abdalla amesema ushirikiano huo utaisaidia
Serikali na wananchi kwa ujumla kuwa na uhakika wa upatikanaji dawa na
kupunguza mzigo wa kutumia gharama kubwa kuagiza dawa.
Amesema
hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha dawa zote zinapatikana bila usumbufu katika Hospitali na vituo vya
afya na kufanikisha malengo yake ya
kuwapatia wananchi huduma bora za afya.
Chanzo
:Zanzibar24
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment