Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Tido Mhando |
DAR ES
SALAAM
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji
Tanzania TBC,Tido Mhando amefikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam kwa
mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka.
Tido Mhando,ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam
Media alifikishwa katika mahakama ya Kisutu jana na kusomewa dhidi mashtaka yake.
Wakili wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania
(Takukuru) Leonard Swai amemwambia hakimu mkazi mkuu Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka matano.
Anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la
Serikali TBC pamoja na kulitia hasara ya shilingi milioni 897.
Mhando anadaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2008
alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC.
Hata hivyo amekana mashtaka yote na kuachiwa
kwa dhamana ambapo kesi imeahirishwa hadi Februari 23 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Chanzo :Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment