Saturday, 27 January 2018

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametangaza kiama kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kuagiza mpaka ifikapo April 30 mwaka huu wahakikishe wamelipa kodi hiyo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi


MWANZA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametangaza kiama kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kuagiza mpaka ifikapo April 30 mwaka huu wahakikishe wamelipa kodi hiyo.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo katika ziara mkoani Mwanza alipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya jiji la Mwanza na kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo la ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi linakamilika kwa wakati.

Aidha amewataka wakuu wa idara za ardhi nchini kusajili hati za viwanja kwa wanaohitaji ardhi kwa kutumia majina yanayotambulika kwenye vitambulisho vya taifa NIDA ili kuepuka udanganyifu ambapo kodi hiyo ipo kisheria.
Waziri Lukuvi pia amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanapima maeneo yote yakiwemo mamlaka za viwanja vya ndege,hifadhi za wanyama na misitu.


Chanzo :Eatv 
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...