KATAVI
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Katavi Hassan Omary amewataka watendaji
wa mahakama kusimamia maadili ya kazi zao katika uwajibikaji wa kuwa tumikia
wananchi katika kutoa maamuzi mbalimbali ya kesi wanazoziendesha ktika maeneo
yao yakazi.
Bwana omary amebainisha hayo wakati akizungumza na mpanda Redio amesema kunabaadhi ya malalamiko ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wananchi yanayo walenga moja kwa moja baadhi ya watumishi wa mahakama katika utekelezaji wa majukumu yao kwa wananchi hasa yale ya ucheleweshwaji wa maauzi ya kesi pasipo na sababu za msingi
Aidha amesisitiza kuwa nivyema wanachi kufahamu kuwa mahakama ndiyo
sehemu sahihi ya kukimbilia pindi wanapoona haki zao zinapolwa na watu wasio
jua taratibu kanuni na sheria za nchi pamoja na hayo amesema muhimili huo wa
utoaji haki nivyema ukaachwa ufanyekazi yake pasipokuingiliwa na Mtu au taasisi
yeyote katika utoaji wa maamuzi mbalimbali ya kesi
Kwa upande wake afisa Tehama wa mahakama hiyo bwana James Kapele amesma
kuwepo kwa mfumo wa kieletroniki katika undeshaji wa kesi mbalimbali kumepunguza
mlundikano wa kesi ambao ulikuwa unajitokeza kabla ya mfumo huo wa kuanza
kutumika hapa nchini.
Chanzo :Paul Mathias
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment