Tuesday, 5 September 2017

Baadhi ya Wajasiliamali wadogo wadogo Mkoani Katavi wameeleza ugumu wa kupata mikopo kuwa kikwazo cha ukuaji wa biashara zao.


MPANDA


Wakizungumza na mpanda redio kwa nyakati tofauti wamesema kuwa  nia ya kutaka kupanua wigo wa biashara ili ziwe natija zaidi kwa jamii na taifa, inawezekana kama urasimu wa upatikanaji wa mitaji utaondolewa katika taasisi za serikali.

Wajasiliamali hao wameongeza kuwa upatikanaji wa mikopo unaweza kuwainua katika ukuaji wa vikundi pamoja na biashara katika kufikia malengo.


 Kila Halmashauri hutenga asilimia kumi kuwezeshwa mikopo kwa uwiano wa asilimia tano kwa vijana na asilimia tano kwa wanawake.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...