Tuesday, 5 September 2017

Kifo cha ugonjwa wa Malaria chawashangaza madaktari Itali.

Vimelea vya Plasmodium Falciparum vinavyobebwa na mbu wanaosambaza malaria vinaweza kuuwa mtu katika kipindi cha saa 24.



Msichana mmoja wa miaka minne amefariki kutokana na malaria ya ubongo kaskazni mwa Itali, eneo ambalo halina ugonjwa huo katika kile ambacho madaktari wanasema ni kisa kisicho cha kawaida.

Sofia Zago alifariki mjini Brescia siku ya Jumapili usiku baada ya kupelekewa huko akiwa na vipimo vya juu vya joto mwilini siku ya Jumamosi.
Italy haina mbu wanaosambaza ugonjwa huo, ukiwa ndio mbaya miongoni mwa magonjwa yote ya malaria.

Lakini baada ya jua kali la mwezi Agosti huenda ugonjwa huo umewasili nchini Italy.
Sofia alikuwa katika likizo na wazazi wake katika eneo la Bibione eneo la kitalii lilipo mji wa Venice.

Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30 kuweza kuona kisa cha ugonjwa wa malaria kilichotoka eneo la Trentino, alisema Dkt Claudio Paternoster ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya usambazaji katika hospitali ya Santa Chiara.

Tangu miaka ya hamsini ,italy haijawahi kupata kisa cha malaria kwa kuwa maeneo wanayozaana hutibiwa.
Kuna uvumi kwamba Sofia huenda alipata malaria hiyo kutoka kwa watoto wawili waliotibiwa katika hospitali ya Trento mnamo tarehe 15 mwezi Agosti .

Waliupata ugonjwa huo barani Afrika na kupona.
Vimelea vya Plasmodium Falciparum vinavyobebwa na mbu wanaosambaza malaria vinaweza kuuwa mtu katika kipindi cha saa 24.

Takriban watu 438,000 walifariki 2015 katika mataifa 95 ya eneo la tropiki ambapo ugonjwa huo ni janga.
#habari toka Bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...