Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Habari cha Bunge,
Spika atapokea ripoti hizo na kisha kuzikabidhi kwa Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa.
Dodoma. Spika wa Bunge,
Job Ndugai kesho atapokea ripoti ya kamati ya maalum mbili zilizoundwa kwa
ajili ya kuchunguza biashara ya madini aina ya Tanzanite na almasi.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa jana na Kitengo cha Habari cha Bunge, Spika atapokea ripoti hizo na
kisha kuzikabidhi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kamati hizo ziliundwa
katika Mkutano wa Saba wa Bunge na Ndugai ambaye alizipa siku 30 kukamilisha
kazi hiyo.
Pia wabunge watapokea
taarifa ya Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo.
Taarifa hiyo inasema
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Namba 3 wa mwaka 2017, Muswada wa
Sheria ya Reli wa Mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno
na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka 2016.
Leo Bunge litaanza kwa
kuwaapisha wabunge saba wa viti maalum wa CUF walioteuliwa hivi karibuni.
Wabunge hao ni Afredina
Apolinary Kahigi, Kiaza Hussein Mayeye , Nuru Awadhi Bafadhali, Rukia Ahmed
Kassim, Shamsa Aziz Mtamba, Sonia Jumaa Magogo, Zainab Mndolwa Amir.
#habari toka mwananchi
#habari toka mwananchi
No comments:
Post a Comment