Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Mpanda Mkoani kesho inatarajia
kutoa hukumu dhidi ya Kigalu Huba mkazi wa kijiji cha Kambuzi wilayani Mpanda
Mkoani Katavi anayekabiliwa na kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha aina ya
kivita ya AK47.
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Mh.Chiganga Tengwa ametoa kauli hiyo
hilo leo mahakamani hapo mara baada ya kusikiliza maelezo ya shahidi wa pande
zote mshtaki na mshtakiwa.
Awali mkuu wa upelelezi mkoani Katavi Emmanuel Parangyo ameiambia
mahakama hiyo kuwa Bw.Humba alipatikana na hatia hiyo Machi 19 mwaka huu katika
nyumba anayoishi ambapo alikuwa akilalamikikiwa na wananchi kwa kujihusisha na
matukio ya uhalifu mara kwa mara.
Aidha Parangyo ameiambia mahakama kuwa mwananchi haruhusiwi kumiliki
risasi au silaha ya kivita kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi
ya Tanzania.
Hata hivyo mtuhumiwa amekana shitaka dhidi yake ya kumiliki risasi
hizo bila kibali huku akiomba mahakama impunguzie adhabu atakapobainika kuwa na
hatia kwa kuwa anategemewa na familia yake pamoja na mama yake mzazi ambaye kwa
sasa ni mgonjwa.
Source:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment