Saturday, 7 April 2018

MKUU WA WILAYA YA MPANDA AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WAFANYABIASHARA BUZOGWE



Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Lilian Charles  Matinga ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wafanyabiasha wa soko la Buzogwe kutokana na kukaidi agizo la kufanya usafi katika maeneo hayo.

Amesema hayo mapema leo alipokuwa akishiriki katika zoezi la usafi katika soko la Buzogwe ambapo ameambatana na maafisa wa jeshi la polisi wakiwemo watumishi wa umma.

Sanjari na hayo miongoni mwa wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wamesema kama serikali itaendelea kuhamasisha usafi mara kwa mara hakutakuwa na hofu ya magonjwa ya milipuko.

Hapo jana mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga aliagiza watumishi wa umma na wananchi kushiriki katika zoezi la usafi kama sehemu ya kumbu kumbu ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume aliyefariki kwa kupigwa risasi Arili 7,1972.

Chanzo: Alinanuswe Edward

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...