Sunday, 10 September 2017

Raila,Uhuru hawatabadilisha wasimamizi wa uchaguzi katika kambi zao.

                                                     Uhuru Kenyatta na   Raila Odinga  


Rais Uhuru Kenyatta na hasimu wake wa kisiasa Raila Odinga wanaendelea kuwatumia makamanda wao walioshiriki kusimamia uchaguzi wa mwezi August 2017 katika kinyang’anyiro cha urais unaorudiwa tena nchini Kenya.
Hata hivyo wanawashirikisha wataalamu wa IT, hatua ambayo imeelezwa imetokana na jinsi teknolojia ilivyokuwa imechangia kuathiri matokeo ya uchaguzi wa August 8; matokeo ambayo yalisababisha kubatilishwa uchaguzi huo na Mahakama ya Juu ya Kenya.
Vyanzo vya habari nchini Kenya vinasema kufuatia umuhimu wa Teknohama (ICT) katika kuendesha uchaguzi, kambi zote mbili zinashindana katika kupata watu wajuzi au makampuni mahiri katika fani hiyo.
Hatua hiyo ni ya kimkakati ili kuhakikisha kuwa hawasalitiwi na vitendo vyovyote vya udukuzi wa seva zao na mifumo yao ya uchaguzi kama ilivyokuwa imebainika kutokea wakati wa uchaguzi wa August 8.
Uchaguzi wa urais nchini Kenya utarudiwa Octoba 17, kama ilivyokuwa imetangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
Katika tamko lake, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati amesema hakutakuwa na uteuzi mpya katika uchaguzi huu.
Chebukati amesema Kiongozi wa NASA peke yake Raila Odinga, na Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na wagombea wenza wao watashiriki.
Mgombea mwenza wa Odinga ni Kalonzo Musyoka na yule wa Kenyatta ni makamu wake William Ruto.
“Tume hiyo inapitia taratibu na hatua zinazohitajika kuendesha uchaguzi huo upya na itawajulisha wadau wote mapema baadae,” 

 Uchaguzi wa nchini kenya utafanyika tarehe 17 mwezi wa 10 mwaka 2017 kama ilivyopagwa
na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.

@habari na voa swahili.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...