Meli ya mizigo iliyokuwa
inapeperusha bendera ya Tanzania imezama nje kidogo ya Pwani ya Oman huku
mabaharia wake wote 20 wakiokolewa. Mabaharia hao waliokolewa na wavuvi
waliokuwa karibu na meli hiyo.
Wizara ya Usafiri na Mawasiliano ya Oman imesema, meli hiyo
iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ilikuwa imebeba mchanga na
vyuma ilizama katika pwani ya Lakabi kusini mwa Oman.
Taarifa ya Wizara hiyo imesema sababu ya meli kuzama ni
tatizo la kuvuja.
Polisi ya Oman imeandika katika ukurasa wake wa Twitter
kwamba meli hiyo iliyokuwa ikitokea mji wa Sharjah wa Umoja wa Falme za Kiarabu
ilikuwa ikielekea nchini Eritrea katika Pembe ya Afrika.
#habari toka mwananchi
No comments:
Post a Comment