Miongoni mwa mambo
yatakayofanyika kwenye Bunge ni kuapishwa kwa wabunge wapya wa Cuf.
Mkutano wa nane
wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza kesho mjini Dodoma.
Kwa
mujibu wa ofisi ya Bunge ratiba ya bunge itatolewa leo baada ya kamati ya
uongozi kukutana na kuamua uwasilishwaji wa mswada iliyopo
Katika
mkutano huo wabunge wa chama cha Cuf wanatarajiwa kuapishwa kutokana na baadhi
ya wabunge kufukuzwa baada ya kukikuka utaratibu na miongozo ya chama hicho
ikiwa ni pamoja na kutohudhuria vikao.
Juzi
mbunge mmoja ambaye alitarajiwa kuapishwa na wenzake kesho Mbunge mteule wa
Viti Maalum Hindu Mwenda alifariki dunia na kuzikwa jana makaburi ya Kisutu.
Naibu
Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema
chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha
Hindu
alifariki dunia ghafla nyumbani kwake Kibada Kigamboni.
Sakaya
amesema Hindu alikuwa ni mpambanaji na mtu mwenye kukijenga chama
hicho kuanzia miaka ya 90 hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.
‘’Hata
ukifika Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema
Sakaya.
“Sijui
niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tuaende Dodoma kuapishwa baada
ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi
(NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.
No comments:
Post a Comment