Kwenye barua waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Yusuf Garaad, alisema kuwa wanamgambo hao wameteka eneo lenye madini ya uranium na wamekuwa wakichimba madini hayo |
Serikali ya Somalia imetuma ombi la
msaada wa kijeshi kwa Marekani, kuwazuia wanamgambo wa al-Shabab kuchimba
madini ya uranium ya kuyatuma hadi nchini Iran.
Kwenye barua waziri wa mashauri ya
nchi za kigeni Yusuf Garaad, alisema kuwa wanamgambo hao wameteka eneo lenye
madini ya uranium na wamekuwa wakichimba madini hayo.
Somalia inatajwa kuwa yenye madini
ya uranium kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la kimataifa la kudhibti
nishati ya nyuklia
Madai hayo hayajathibitishwa rasmi
kuhusu vile uchimbaji huo wa madini ufanywa au ni kwa njia ipi al-Shabab
inatuma madini hayo kweda Iran.
Islamic State wakati limefahamika
kuwa na uhusiano wa muda mrefu na al-Qaeda.
Ilisema kuwa tatizo la sasa ni kubwa
hata kukishinda kikosi cha Muunganoi wa Afrika kilicho nchini Somalia.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni
haijajibu barua hiyo lakini vyombo vya habari vinasema kwa Marekani
ilithibitisha kuipokea barua hiyo.
No comments:
Post a Comment