Wataalamu wa kutegua
mabomu wa Ujerumani wakiwa wameketi karibu na bomu hilo Jumapili
Wataalamu
wa kutegua mabomu mjini Frankfurt, Ujerumani siku ya Jumapili walifanikiwa
kutegua bomu kubwa ambalo halikuwa limelipuka ambalo liliangushwa wakati wa
Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Bomu
hilo la tani 1.4 kutoka Uingereza liligunduliwa katika eneo la ujenzi Jumatano.
Habari
hizo zilipokelewa kwa shangwe na watu zaidi ya 65,000 ambao walikuwa
wamehamishwa maeneo yao kwa sababu za kiusalama baada ya bomu hilo kuteguliwa.
Hiyo
ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuhamishwa tangu kutokea kwa Vita Vikuu vya
Pili vya Dunia nchini Ujerumani, na shughuli hiyo ilihusisha mamia ya maafisa
wa serikali.
Maeneo
ambayo watu walihamishwa yalikuwa katika mtaa wa Westend, na ni pamoja na
hospitali kadha, nyumba za kuwatunza wagonjwa na hata katika Benki Kuu ya
Ujerumani.
Inaaminika
kwamba kuna mamia ya maelfu ya mabomu ya wakati wa vita ambayo hayakulipuliwa
ambayo yametapakaa kote Ujerumani.
Bomu hilo la tani 1.4 kutoka
Uingereza lilipatikana katika eneo la ujenzi Jumatano . Watu waliohamishwa
wanatarajiwa kuruhusiwa kurejea makwao karibuni.
Barabara
zilifungwa na maafisa wa polisi Jumapili asubuhi
Polisi wakitumia helikopta na kamera za kupima viwango vya joto
walipaa angani eneo hilo wataalamu wa kutegua bomu walipokuwa wakiendelea na
kazi yao
No comments:
Post a Comment