Korea Kusini imefanya majaribio leo Jumatatu
Korea Kusini inasema kuwa kuna
dalili kuwa Korea Kaskazini inapanga majaribio zaidi ya makombora hususan
makombora ya masafa marefu.
Maafisa wa ulinzi wamekuwa
wakilishauri bunge mjini Seoul baada ya Korea kulifanyia jaribio bomu la
nyuklia mwioshoni mwa wiki.
Korea Kusini imejibu kwa kufanya
majaribio kwa kurusha makombora kwa kutumia ndege na kutoka ardhin
Marekani imeonya kuwa tisho lolote
kwake na kwa washirika wake litajipigwa vikali kijeshi.
Korea Kusini inasema kuwa
ililifanyia majaribio bomu la haidrojeni ambalo linaweza kuwekwa kwa kombora la
masafa marefu.
Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa
linatarajiwa kufanya kikao cha dharura baadaye leo kujadili hatua za kuchukua.
Chang Kyung-soo, ambaye ni afisi
kutoka wizara ya ulinzia aliliambia bunge, "tunaendelea kuona dalili za
uwezekano wa makombora zaidi ya masafa marefu. Pia tunaweza kutabiri kuwa Korea
Kaskazini huenda ikarusha kombora la masafa marefu.
Wizara hiyo pia ililiambia bunge
kuwa huenda Marekani ikapeleka manowari wa nyuklia ya kubeba ndege katika rasi
ya Korea.
No comments:
Post a Comment