Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha
kwa wazazi wao baada ya kupewa Shlingi millioni tatu.
Matukio ya utekaji
watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa
miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika mji wa Katoro
wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji.
Alisema
wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha
walichotakiwa kumpa.
Samson
alisema alianza ‘shughuli’ hiyo ya utekaji watoto kutokana na mahitaji ya fedha
na kwamba, aliacha shule akiwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lutozo
iliyopo Katoro.
“Naishi
na wazazi wangu, lakini nao ni masikini, nilifanya hivi ili nipate fedha na
nilikuwa nikimchukua mtoto naandika ujumbe kwenye karatasi, naandika na namba
ya simu napeleka karibu na familia ili wanitafute,” alisema Samson.
Awali,
kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema walimkamata kijana
huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mjini Katoro juzi saa
mbili usiku.
Mwabulambo
alisema polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha walifanya
uchunguzi na kubaini mtuhumiwa alikuwa Katoro.
Alisema
walipata taarifa za kutekwa Justin Ombeni (2) Septemba Mosi nyumbani kwao
katika eneo la Shilabela ambako mtuhumiwa alikwenda na kuwakuta watoto wanne
wakicheza nyuma ya nyumba. Alisema aliwagawia pipi na kuondoka na Justin.
Kamanda
huyo alisema polisi ilipata taarifa kuwa kijana huyo yupo chumba namba 103
katika nyumba hiyo ya wageni ambako waliweka ulinzi kuizunguka.
Alisema
walipoingia katika chumba hicho walimkuta akiwa na mtoto huyo.
Mwabulambo
alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Ombeni
Mshana ambaye ni baba wa Justin alisema mtekaji huyo alimpatia ujumbe mtoto wa
jirani uliomtaka kutuma Sh4 milioni na walipokuwa wakiwasiliana na mtuhumiwa
alishusha kiwango hadi Sh1 milioni. Alisema polisi walimtahadharisha kwamba
asitume fedha hizo.
Kamanda
Mwabulambo alisema tukio la kutekwa Justin ni la pili katika kipindi cha miezi
minne baada ya mwingine kutekwa. Kesi kuhusu tukio hilo la kwanza inaendelea
mahakamani baada ya mtoto kupatikana.
Katika
hatua nyingine, kikosi kilichoundwa na wananchi mkoani Arusha kikiongozwa na
mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Kata ya Olasiti, Daudi Safari na familia za
watoto wawili waliotekwa kimewakamata watuhumiwa wawili na kuwafikisha polisi.
Watoto
hao ambao bado hawajapatikana ni Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza
shule ya msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3).
Wakizungumza
jana nje ya kituo kikuu cha polisi Arusha baada ya kuwafikisha kituoni
watuhumiwa hao, Safari na wazazi wa watoto hao, David Njau na Salim Kassim
walisema kwa nyakati tofauti wameanzisha msako baada ya kuona siku zinakwenda
bila watoto kupatikana.
Moureen
alitekwa Agosti 21 saa 11 jioni akiwa anacheza nyumbani kwao eneo la Olasiti,
wakati Ikram alitekwa Agosti 26 saa 12 jioni akiwa anacheza na watoto wenzake
nyumbani kwao, Burka - Olasiti.
Safari
alisema wamemkamata mtu mmoja (jina linahifadhiwa) ambaye simu yake ilitumiwa
na watekaji kuomba fedha kwa mzazi wa Ikram Salim.
Alisema
pia wamemkamata wakala wa fedha wa kampuni moja ya simu (jina tunaihifadhi)
aliyetoa Sh300,000 kwa watekaji baada ya fedha kutumwa na mzazi wa Ikram.
Imeelezwa kuwa wakala huyo amekamatwa kwa kuwa fedha hizo zilitolewa pasipo
kuorodheshwa popote na mpokeaji hakuonyesha kitambulisho chochote.
Akizungumzia
operesheni hiyo, Njau alisema hawatapumzika mpaka watoto wao wapatikane.
Alisema
ufuatiliaji walioufanya kupitia minara ya kampuni za simu unaonyesha wahusika
walikuwa eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha walipopiga kuomba Sh4.5 milioni ili
wamwachie Doreen na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya Ikram.
Watekaji
hao kupitia ujumbe waliotuma nyumbani kwa Njau walidai kama wasipopewa fedha
wangempoteza mtoto huyo japokuwa hawana nia hiyo.
Kassim
Salim ambaye ni babu wa Ikram alisema, “tunaendelea kuomba msaada zaidi kwa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyombo vya dola watusaidie tuwapate
watoto wetu.”
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema juzi kuwa watu watatu
wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo akiwapo dereva wa bodaboda mkazi wa
Olasiti aliyetumwa kuwarejesha watoto wawili waliokuwa wametekwa.
Matukio ya utekaji
yalianza kuibuka Agosti 21 baada ya kutekwa watoto wanne. Watoto wawili Ayoub
Fred na Bakati Selemani wakazi wa eneo la FFU, kata ya Murieti jirani na kata
ya Olasiti walirejeshwa.
No comments:
Post a Comment