HALAMSHAURI ya Manispaa ya Mpanda
imesema inatarajia kuanzia kuchimba kisima cha maji katika Machinjo yaliyopo
Kata ya Mpanda Hotel kama hatua ya utatuzi wa changamoto ya uhaba wa maji mara
kwa mara.
Hatua hiyo imethibitishwa na
Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu wakati akizungumza na
Mpanda Radio kufuatia Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Manispaa ya Mpansa
(MUWASA) kusema kuwa haina maji ya kutosha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mamlaka
ya maji na usafi wa mazingira Manispaa ya Mpanda Mhandisi Zacharia Nyanda leo
akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema tatizo la uhaba wa maji
katika machinjio ya Mpanda Hotel inatokana na kiasi kidogo cha maji kilichopo
katika vyanzo.
Baadhi ya wafanyakazi wanaofanya kazi
katika machinjio ya Mpanda Hotel ambao hawakutaka kutaja majina yao kwa madai
kuwa wao siyo wasemaji,wamesema siku ya jana walishindwa kuchinja ng’ombe
kutokana na ukosefu wa maji ambapo wamesema tatizo hilo limekuwa likitokea takribani
mara nne kwa mwezi ambapo imeelezwa kuwa tatizo hilo limekuwepo kwa muda mrefu.
Mwaka 2015 Mamlaka ya Chakula na dawa
nchini TFDA ilifunga machinjio ya Mpanda Hotel kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo uchafu uliotokana na tatizo la ukosefu wa maji kwa kuwa uwepo wa uchafu
ulikuwa ukihatarisha afya za walaji.
Na.Issack Gerald
No comments:
Post a Comment