Inadaiwa
kuwa askari huyo pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano tangu Agosti 27
wakati kikosi maalum cha polisi kilipozingira nyumba aliyopanga.
Arusha.Wakati Mtuhumiwa
wa matukio ya utekaji watoto, Samsom Petro (18), ambaye jana alifikishwa Arusha
kwa ajili ya kuonyesha sehemu alipowaficha watoto, amebainika kuwa anaishi na
kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa.
Inadaiwa kuwa askari
huyo pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano tangu Agosti 27 wakati kikosi
maalum cha polisi kilipozingira nyumba aliyopanga.
Petro, ambaye
alikamatwa juzi akiwa Katoro mkoani Geita, anatuhumiwa kuwateka watoto wawili,
Moureen David(6) na Ikram Salim(3) na hadi jana jioni alikuwa ameandamana na
polisi katika eneo la Njiro ambako alidai aliwatelekeza watoto hao.
Akizungumza na
Mwananchi, Lina Kajuna ambaye ni mmiliki wa nyumba ya aliyekuwa amepanga askari
huyo wa FFU, alisema ana miaka miwili tangu ampangishe.
Kajuna alisema
mtuhumiwa wa utekaji, Samson Petro alifika Arusha mwezi Juni na amekuwa akiishi
na kaka huyo na tangu amefika amekuwa akimuona kuwa na tabia ambazo sio nzuri,
kama wizi wa kuku.
“Alipofika muda mfupi
tulianza kuona matukio ya wizi nikaibiwa kuku na pesa mimi nikamlalamikia kaka
yake lakini akasema tuendelee kumchunga,”alisema
Alisema baada ya hali
ya wizi kuendelea, alikwenda kulalamika kwa balozi wa eneo wanaloishi ambalo ni
Mtaa wa Olkeria, Daniel Kichau kutaka wamchunguze.
Hata hivyo, alisema
wakati akichunguza, ndio matukio ya utekaji yakaanza na tangu Agosti 25
alitoweka nyumbani hadi jana walipopata taarifa kuwa amekamatwa.
Akizungumzia tukio
hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari alisema jana kuwa kikosi
chao cha wananchi walifika kwenye nyumba hiyo na kubaini alikuwa anaishi na
askari huyo wa FFU .
“Tumemuhoji mama mwenye
nyumba ametupa ushirikiano mkubwa na ni kweli Samson alikuwa anaishi kwenye
nyumba yake na kaka yake ambaye alikamatwa tangu Agosti 27,” alisema.
Katika msako wa jana, polisi
walikwenda peke yao na mtuhumiwa na kuwaacha wazazi wa watoto hao wakiwasubiri
kituo kikuu cha polisi. Baadhi ya askari walisema wanaendelea na msako wa
watoto hao.
No comments:
Post a Comment