Taarifa kutoka
Zimbabwe zinasema kuwa kumefikiwa makubaliano yanayompa kinga ya kutoshitakiwa
aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, na pia kumuhakikishia usalama wake.
Chanzo cha ndani kwenye mazungumzo hayo kinasema kuwa hayo yamefikiwa kama sehemu ya makubaliano ya kumfanya Mugabe akubali kuachia madaraka, baada ya miaka 37.
Mugabe, mwenye umri wa miaka 93 aliyelazimika kujiuzulu Jumanne wiki hii baada ya wabunge wa nchi hiyo kuanzisha mchakato wa kumuondoa madarakani, hajaonekana hadharani tangu alipolihutubia taifa Jumapili iliyopita na kukataa wito wa kujiuzulu.
Inaelezwa kuwa kiongozi huyo bado yuko mjini Harare pamoja na mkewe, lakini haijafahamika wazi zaidi ni kwa mazingira yapi.
Makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo, Emerson Mnangagwa, aliyefutwa kazi na Mugabe mapema mwezi huu, anatarajiwa kuapishwa hapo kesho Ijumaa, baada ya kurejea jana nchini humo.
SOURCES:BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment