Picha ya kituo cha KCNA) ya Agost 29, 2017, ikionesha kituo cha majaribio ya makombora cha Korea Kaskazini |
Korea
Kaskazini imeonekana kufanya jaribio la sita la nyuklia leo Jumapili, na
wachunguzi wamepima "mlipuko" uliotokea na kusema una ukubwa wa
karibu 6.3 karibu na eneo lake kuu la majaribio ya makombora yake na
kusababisha mvutano kuhusu nia yake ya kuwa na silaha za nyuklia
Mlipuko
huo umekuja saa kadhaa tu baada ya Korea Kaskazini kusema kuwa imetengeneza
bomu la hidrojeni ambalo linaweza kupakiwa kwenye kombora jipya la kimataifa la
kimataifa , vyombo vya habari vya serikali vimearifu leo Jumapili, na kuongeza
mvutano kuhusu mpango wake wa slaha za nyuklia.
Pyongyang
inayojihami kwa silaha za nyuklia, kwa muda mrefu imetafuta njia za kufikisha
mabomu ya atomic kwa Marekani, ambayo ni adui yake mkubwa..
Waziri
Mkuu wa Japani Shinzo Abe amesema kuwa jaribio la sita la nyuklia la Pyongyang
"halikubaliki kabisa.
No comments:
Post a Comment