Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya
mahakama ambayo inahitaji 'marekebisho'.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema
kuwa taifa hilo lina 'matatizo' na idara ya mahakama ambayo inahitaji
'marekebisho'.
Alikuwa akizungumza katika hotuba
uliopeperushwa moja kwa moja na runinga siku moja tu baada ya mahakama ya juu
kubatilisha uchaguzi wake na kuagiza uchaguzi mpya katika kipindi cha siku
sitini.
Rais Kenyatta alisema kuwa
ataiangazia idara ya mahakama ,mbali na kurejelea ujumbe wake kwamba
atauheshimu uamuzi wa mahakama hiyo.
Wameonya kuikabili idara hiyo baada
ya uchaguzi
''Hata iwapo wewe ni mjinga jiulize
hivi, matokeo ya uchaguzi wa MCA yalikubaliwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali
mengi, matokeo ya maseneta na ya wabunge nayo yalitangazwa na tayari
wameapishwa na hakuna mtu aliyeuliza maswali. Matokeo ya magavana yalitangazwa
na hakuna mtu aliyeuliza maswali ,sasa inakuwaje watu wanne wanaamka na kusema
kuwa matokeo ya urais yaliotangazwa yalikuwa na dosari.
Kivipi, kivipi? aliuliza rais Kenyatta
katika ikulu ya rais alipokutana na viongozi wa chama cha Jubilee
waliochaguliwa.
Rais huyo aliyeonekana kuwa na
hasira alionya kukabiliana na majaji hao wa mahakama ya juu atakapochaguliwa.
Mkutano wa wanachama wa Jubilee
uliofanyika katika Ikulu ya rais
''Tuna matatizo hapa. Mwanzo ni nani
aliyewachagua? tuna tatizo na lazima turekebishe'', alisema.
Amesisitiza kuwa ijapokuwa
anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo ya juu na kwamba alikuwa tayari kushiriki
katika uchaguzi mwengine alisema kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa na
makosa.
''Mahakama ya juu iliketi chini
ikaamua kwamba hiyo ndio yenye nguvu zaidi ya Wakenya milioni 15 walioamka
alfajiri na kupanga foleni na kumpigia mgombea wa urais waliomtaka''.
Rais
Uhuru Kenyatta akiwahutubia viongozi wa chama tawala ha Jubilee siku moja baada
ya uchaguzi wake kubatilishwa na mahakama
''Mahakama ya juu haiwezi kufutilia
mbali maono ya Wakenya.Na tutaliangazia swala hili.Niangalieni machoni na
museme iwapo upendo wangu wa Wakenya kuishi kwa amani ndio unaonekana kuwa
uoga, hatuogopi''.
No comments:
Post a Comment