Wakazi wa eneo la Luhafwe
katika kata ya Tongwe Halmashauri ya
wilaya ya Mpanda Mkoa wa katavi
wameanzisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa ya shule ya msingi luhafwe.
Wakizungumnza katika
mkutano wa hadhara ulio itishwa na Mkuu wa wilaya hiyo Salehe Mbwana
Mhando Wakazi hao wamesema wameguswa na changamoto ya
ukosefu wa huduma za kijamii hususani Elimu ndiyo maana wameamua kuchangia shilingi millioni sita kama mchango wao katika kuunga juhudi za
maendeleo katika eneo hilo.
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando amesema niwajibu wa kila mwanachi
kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kutatua tatizo la ukosefu wa miundo
mbinu imara katika huduma za jamii kama vile
elimu.
Serikali ya awamu ya tano
kupitia mradi wa Equip imeunga mkono jitihada za wananchi kwa kupeleka kiasi
cha Tsh mil 60.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa,ofisi moja ya
walimu na ujenzi wa vyoo.
Awali eneo hilo la
Luhafwe halikuwa eneo rasmi la makazi lakini kwa sasa eneo hilo lililopo katika
eneo la uwekezaji la halmashauri ya wilaya ya Mpanda limerasmishwa rasmi kuwa
eneo la makazi.
CHANZO:PAUL MATHIAS
No comments:
Post a Comment