Mpango
wa Matumizi bora ya ardhi umeelezwa kuwa ni changamoto katika jamii kutokana na
ongezeko la vijiji katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi.
Kusundwa Wamarwa mtetezi wa haki za binadamu
katika makundi ya asili kanda ya magharibi amesema hali hiyo inasababisha kushindwa kutenga maeneo ya shughuli za
binadamu pamoja na makazi .
Bw.
Wamarwa amesema changamoto hizo mara nyingi hutokana na wananchi
kutoelewa mmiliki wa ardhi ya kijiji ni nani wakifiri ni mwenyekiti wa
kijiji kumbe ni wanakijiji wenyewe .
Licha
ya kuwepo mpango wa matumizi bora ya ardhi serikali haina budi kutoa elimu kwa wananchi juu ya
malengo ya matumizi hayo kwa manufaa ya
taifa ili kuepusha migogoro ya ardhi .
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment