Monday, 9 April 2018

SHEKHE MUNA AFAFANUA MAREKEBISHO YA KATIBA




Katibu wa baraza la waislamu  Tanzania BAKWATA  wilaya Mpanda Mkoani Katavi Sheikh Omary Ally Muna Ametolea ufafanuzi marekebisho ya katiba yaliyofanywa na baraza hilo.

Sheikh Muna amesema marekebisho hayo yamefanywa ili kuziba mianya yote ya ufisadi wa mali za Waislamu na kuingiza kipengele kinachoagiza kutoruhusiwa kuuzwa kwa mali yoyote iliyo chini ya Wakfu wa dini hiyo.

Katiba hiyo pia imefanyiwa marekebisho makubwa na muhimu ambayo yanafuta mfumo wa awali wa Masheikhe wa Mikoa, Wilaya, Kata na Maimamu wa Misikiti kupatikana kwa njia ya uchaguzi na sasa wanateuliwa.

Mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na falsafa mpya ya Bakwata Mpya, Jitambue, Badilika ni uamuzi uliofikiwa wakati wa Mkutano Mkuu wa baraza hilo uliofanyika Machi 31 na Aprili 1, mwaka huu, mjini Dodoma.
Chanzo:Haruna  Juma

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...