Kata ya Kakese iliyopo Halmashauri ya Manispaa
ya Mpanda mkoani Katavi imetekeleza mpango wa ugawaji wa asilimia kumi kwa
vikundi vya wanawake na vijana.
Akizungumza na Mpanda Fm kwa njia ya simu afisa
Mtendaji kata ya Kakese Lauben Kasomo amesema mapaka sasa shilingi milioni
mbili zimetolewa kwa vikundi viwili vya wanawake .
Katika hatua nyingine amebainisha uwepo wa
hamasa kubwa miongoni mwa wananchi katika kuunda vikundi kama inavyo takiwa na
serikali kwamba ili kurahisisha utoaji huduma kwa jamii kwa njia ya vikundi.
Aidha ameongezea kuwa swala la ugawaji mikopo
katika vikundi hivyo limekumbwa na changamoto nyingi ikiwemo bajeti kutokidhi
mahitaji hasa kutokana na ongezeko la watu.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Mkaguzi mkuu wa wa
hesabau za serikali Prof Juma Assad amezionya halmashauri kuacha kususua katika
kutekeleza utoaji wa asilimia kumi kwa makundi ya vijana na wanawake.
Chanzo:Ezelina
Yuda
No comments:
Post a Comment