Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutoogopa
kutoa kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa lengo la kuleta maendeleo ya
mkoa kwa ujumla.
Afisa Tawala mkoa ambaye pia ni Mwenyekiti wa
kamati ya malalamiko mkoa David Muya ametoa ufafanuzi wakati akizungumza na
mpanda redio kuhusu utaratibu wa kupokea kero mbalimbali zinazowakabili wananchi
Muya
amewatoa wasiwasi wananchi kua kila atakeyifika atasikilizwa na kero
zake kutatuliwa kwa wakati kutokana na madawati maalumu ya wasimamizi kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu
Raphael Muhuga anatarajia kusikiliza kero za wananchi april 14 mwaka 2018 siku ya Jumamosi katika viwanja vya Azimio.
Chanzo:Allynanuswe Edward
No comments:
Post a Comment