Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi
wamewashauri viongozi wa serikali wa serikali ya awamu ya tano kuenzi kifo cha
Wazairi Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine kwa kupeleka huduma muhimu za
kijamii kwa wananchi ikiwemo maji.
Wakazi hao wametoa kauli hiyo kwa
nyakati tofauti wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu kumbukumbu ya miaka
34 ya kifo cha waziri mkuu hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki Apriki
12,1984.
Aidha wamesema ni kiongozi
aliyechukia uhujumu uchumi,rushwa,ufisadi huku akishiriki vema kuandaa majeshi
wakatio wa vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda mwaka 1978.
Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine
aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili Februaei 13 mwaka 1977 hadi Novemba 7 mwaka
1980 na Februari 24 mwaka 1983 hadi kifo
chake kwa ajali ya gari Mkoani Morogoro akitokea Bungeni Dodoma kuelekea Jijini
Dar es salaam.
Chanzo:Isack
Gerald
No comments:
Post a Comment