Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi imetanga
zaidi ya ekari elfu mbili kwa ajili ya wafugaji waliopo katika eneo la Luhafwe
katika kata ya Tongwe.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo
Salehe Mbwana Muhando wakati akizungumza
na wafugaji wa eneo hilo amesema serikali kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri imetenga eneo la malisho ili kuepusha usumbufu kwa wafugaji
kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho ya mifugo yao
Aidha Mhando amewaagiza maafisa kilimo na
ufugaji wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa eneo la luhafwe kufanya sensa ya utambuzi wa mifugo katika
eneo hilo ili kuwa na idadi kamili ya mifugo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafugaji wilaya
ya Tanganyika Mussa Kabushi amewaomba wafugaji kuanzisha umoja utakao sajiliwa
kisheria ili kurahisisha utatuzi wa changamoto kwa wafugaji.
Chanzo:Paul Mathius
No comments:
Post a Comment