Mratibu wa Tarura Mkoa Katavi Zuberi Kilenza
Wakala wa barabara za
mjini na vijijini TARURA mkoani Katavi imesema kinachokwamisha baadhi ya
barabara za maeneo mbalimbali kukamilika
ni kutokana na kutumia fedha za bajeti kulipa madeni.
Akizungumza na Mpanda Radio mratibu wa Tarura Mkoa Zuberi
Kilenza amesema baada ya kulipa mdeni hayo zimebaki shilingi Bilioni mbili na
milioni mia tatu kwa ajili ya matengenezo
ya kawaida ya muda maalumu ,madaraja ,makaravati na mifereji.
Kilenza
amesema kuna mikataba kumi na moja
kwenye halmashauri tano za mkoa wa Katavi ambapo wakandarasi wanaendelea
na utengenezaji wa barabara hizo.
Kwa
mujibu wa tafiti zilizofanywa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa hivi karibuni unaonyesha kila mwaka
ni wastani wa asilimia 30 pekee za barabara za Mjini na vijijini ndizo hukamilika
Chanzo:Ester
Baraka
No comments:
Post a Comment