Eneo la mto Koga Lilivyo kufuatia mvua za masika zinazoendela kunyesha hali iliyosababisha bara bara ya Tabora Katavi kufungwa
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amesema barabara ya
Mpanda–Tabora
imefungwa kwa muda usiojulikana kuanzia Aprili 14,2018.
Muhuga ametoa kauli
hiyo katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika uwanja wa Azimio mjini
Mpanda kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi ambapo hata hivyo mkutano huo
umeahirishwa baada ya mvua kunyesha na kupangwa kuitishwa baadaye ili kujibu
malalamiko ya wananchi.
Muhuga amesema
barabara hiyo imefungwa baada ya maji kujaa barabarani kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha na hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri.
Kwa upande wake mkuu
wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi
Amani Mwakalebela amesem kutokana na barabara kuharibika kwa kiasi
kikubwa,wenye mabasi watalazimika kusafirisha abiria kupitia mkoani Kigoma au
Mbeya.
Mwaka 2016 barabara
ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo
karibu watu kumi walipoteza maisha baada ya gari kusombwa na maji.
Chanzo:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment