Wakazi wa kijiji cha Katsunga Machimboni Halmashauri
ya Nsimbo Mkoani Katavi wamesema wanapata fursa ya kuwahoji viongozi wao juu ya
masuala mbalimbali ya maendeleo katika kijiji hicho.
Mpanda Redio
imefika kijijini hapo ambapo wakazi hao wamebainisha kufika kwa viongozi wao
mara kadhaa na kuwauliza kuhusu upatikanaji wa maji,zahanati na umeme.
Mwenyekiti wa
kijiji hicho Lukas Kumpamba amesema wanapokea maoni ya wananchi kupitia sanduku
la maoni na mikutano mbalimbali ya hadhara ambapo kwa sasa wako katika ufumbuzi
wa changamoto ya zahanati.
Kijiji cha
Katisunga Machimboni kina jumla ya wakazi 6000 kwa mujibu
wa sensa iliyofanyika hivi karibuni kijijini hapo.
Chanzo:Ester
Baraka
No comments:
Post a Comment