Mwongozo
huo umetolewa na kaimu mkurugenzi wa utafiti mafunzo na ugani katika wizara
ya mifugo na uvuvi,Dk. Erastus Mosha wakati wa utoaji elimu wa zoezi
hilo. Amesema sehemu ambayo ni salama na isiyo na madhara ya upigaji chapa
katika zao la ngozi ni mguu wa nyuma kulia mwa mnyama juu kidogo ya goti.
Kwa
uapnde wake afisa mifugo manispaa ya Dodoma, Kiboma John,amesema zoezi hilo
linatarajiwa kufikiwa na kata 40 za manispaa hiyo lakini linakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo la uhaba wa fedha, vitendea kazi na rasilimali
watu.
SOURCES:eatv
No comments:
Post a Comment