Vijana Mkoani Tabora wametakiwa kuacha tabia ya kukaa vijiweni na kusikiliza maneno ambayo hayawasaidii wala kuwafundisha namna ya kupata maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika maeneo mbalimbali
ya Kata za Wilaya ya Kaliua kwenye zoezi la uhamasishaji wa kilimo cha
kisasa cha zao la Pamba na mazao mengine.
Aidha
mkuu huyo wa mkoa amewataka vijana kutumia muda wao kujiajiri katika sekata ya
kilimo na uzalishaji wa pamba pamoja na mazao mengine yatakayowasaidia
kujipatia kipato na kuinua maisha yao.
SOURCES:eatv
No comments:
Post a Comment