Watu wapatao 235 wameuawa na wengine 109 kujeruhiwa katika
shambulio linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wa itikadi kali katika msikiti
mmoja wa Rasi ya Sinai.
Kufuatia tukio hilo linatoltajwa kuwa ni shambulio baya zaidi
kuwahi kutokea nchini Misri katika miaka ya hivi karibuni,Rais wa Misri
Abdel-Fattah al-Sissi ametoa ahadi ya adhabu kali dhidi ya wahusika aliowataja
kuwa ni magaidi.
Mashambulizi yalianza muda mfupi baada ya sala ya Ijumaa,ambapo
wanamgambo hao walipotumia vilipuzi katika msikiti wa al-Rawdah.
Gazeti binafsi la al-Masry al-Youm limeripoti kuwa zaidi ya
watu 20 waliokuwa wamebeba silaha walihusika katika shambulio hilo na kwamba
wengi wao wameuawa baadaye katika mashambulizi na vikosi vya usalama.
Ulimwengu umelilaani shambulio hilo la jana ambapo Misri imekuwa ikipambana na uasi Kaskazini mwa Sinai tokea jeshi lilipompindua rais Mohammed Morsi mwaka 2013.
SOURCES:dw,
No comments:
Post a Comment