Maiti za watu watano zilizokatwa vichwa zimepatikana katika
kijiji kimoja cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kaskazini mwa Kivu, eneo
ambalo limeathiriwa na vurugu za kikabila.
Maiti hizo zimegunduliwa katika kijiji cha Kibirizi, kilomita
200 kaskazini-magharibi mwa mji wa Goma, katika eneo la Rutshuru linalopakana
na Uganda.
Mkuu wa kijiji hicho,Arnold Kakule ameliambia shirika la
habari la AFP kwamba eneo hilo limekuwa likishuhudia mapigano ya mara kwa mara
kati ya Wahutu, wanaohusishwa mara nyingi na kundi la waasi wa Rwanda FDLR na
makundi ya Nande na Hunde.
Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo
limekumbwa na machafuko ya kikabila kwa zaidi ya miaka 20 huku makundi tafauti
yakigombania udhibiti wa madini na rasilmali nyinginezo.
No comments:
Post a Comment