Friday, 24 November 2017

Baadhi ya wafanyabiashara wamanispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba mamlaka ya mapato TRA kutoa elimu juu ya ulipaji.



 Na Haruna Juma

Baadhi ya wafanyabiashara wamanispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba  mamlaka ya mapato TRA kutoa elimu juu ya ulipaji.

Wakizungumza na mpanda radio kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wamesema kuwa  elimu inayotolewa haikidhi mahitaji hali inayowafanya baadhi yao kutoelewa viwango sahihi vya kodi kulingana aina ya biashara.

Kwa upande wake meneja wa TRA Mkoa wa katavi Enos Ngimba amesema mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wafanya biashara kabla ya kuanzisha ili kuondoa usumbufu usio wa lazima.

Hata hivyo Bw,Ngimba ameelezea tatizo la wafanyabiashara  kuto udhuria katika Semina zinazo andaliwa kwaajili ya kujengeana uelewa wa Elimu kwa mlipa kodi pamoja na tozo.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...