Friday, 24 November 2017

Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,imesema haina fungu



 

Na Haruna Juma

Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,imesema haina fungu maalumu kwa ajili ya mikopo ya fedha kwa makundi ya watu wenye ulemavu pamoja na wazee.

Hatua hiyo imebainishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa hamashauri hiyo Bi.Halima Kitumba wakati akizungumza na Mpanda radio kuhusu namna wanavyoagawanya mikopo kwa makundi mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi.

Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018,tayari Halmashauri imetumia zaidi ya shilingi milioni sitini na moja katika kipindi cha mwezi Julai hadi Oktoba mwaka huu.

Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ina vikundi zaidi ya 90 vya wajasiliamali wanawake na vijana vinavyonufaika na mikopo.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...