Meya wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Willium Mbogo amesema wameweka mikakati ya kuboresha miundombinu ya watu wenye ulemavu ili waweze kufikia malengo yao.
Willium Mbogo
Na Haruna Juma
Meya wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Willium Mbogo amesema wameweka
mikakati ya kuboresha miundombinu ya watuwenye ulemavu ili waweze kufikia malengo yao.
Amebainisha hayo wakati akizungumza na Mpanada Redio na kusema kuwa
halmashauri inatambua watu wenye ulemavu na tayari imeanza kuboresha mazingira
katika maeneo mbalimbali ili waweze kupata huduma bila shida.
Ameeleza kuwa hapo awali mazingira ya watu wenye ulemavu yalikuwa
hayawapi fursa ya kufika katika maeneo yote jambo ambalo limekuwa chamgamoto
kwao katika dhana ya kimaendeleo.
Hivi karibuni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu aliuambia
umma kuwepo kwa mkakati wa kutenga asilimia 2% kwajili ya walemavu kutoka
katika mapato ya ndani.
No comments:
Post a Comment