Friday, 24 November 2017

Watu 10 wamefariki na wengine 24 kujeruhiwa Mkoani Singida


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba


Watu 10 wamefariki na wengine 24 kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Hiace, kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Noah katika eneo la Ihuka wilayani Ikungi Mkoani Singida.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa gari aina ya Toyota Hice T.581 BBV kulifuata gari aina ya Toyota Noah namba T.423 CFF na kusababisha vifo na majeruhi.

Mganga wa zamu katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu Puma Singida, John Mmary amethibitisha kupokea Miili ya marehemu hao pamoja na Majeruhi wa ajali hiyo ambao wengi wao walikua katika gari aina ya toyota Hiace.

Magari yaliyo gongana aina ya Hice inadaiwa lilikuwa limewabeba maharusi pamoja na ndugu zao huku gari aina ya Noah ilikuwa imewabeba watu walio kuwa wakitokea kwenye msiba.

 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...