Wananchi mkoani katavi hususani wilaya ya
Tanganyika wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhali ikiwa na kutoa taarifa
sehemu husika wanapohisi kuwa na dalili moja wapo za ugonjwa wa ebola ili
huduma sahihi itolewe.
kirusi cha ugonjwa wa Ebola |
Tahadhali hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri
ya wilaya ya Mpanda Selemani Mtenjela ambapo pia amewatoa hofu wananchi kwa
kuwa ugonjwa huo bado haujaingia nchini.
"Tumeanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi kuhusu ugonjwa huu, lakini pia kuwaondoa hofu ili waendelee na shughuli zao huku wakichukua tahadhali," tunachukua tahadhali kwa kuwa mkoa wetu hasa wilaya ya Tanganyika imepakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambako shirika la Afya duniani wamethibitisha kutokea kwa visa vya watu kukutwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo,"amesema Mtenjela.
Amesema kuwa ni vyema wananchi wakaendelea na
shughuli zao huku wakizingatia maelezo ya
wataalamu kwani ugonjwa wa ebola madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na
kupoteza maisha.
Amezitaja dalili za ugonjwa huu kuwa ni
mgonjwa kulalamika kichwa kukosa nguvu ini kudhofika na kutokwa na damu sehemu
za mwili zilizo wazi na kuwa ujitokeza baada ya siku tano hadi 21 tangu
kuambukizwa.
Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo mwezi April 22 mwaka huu lili tangaza kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya
kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo mwaka 2014, mripuko wa ugonjwa huo ulidhibitiwa kwa
haraka ingawa watu 49 walifariki nchini humo.
No comments:
Post a Comment