Friday, 8 September 2017

Kimbunga Irma chaendelea na uharibifu mkubwa huko Caribbean.



_97690837_mediaitem97690836Haki miliki ya picha
Image captionIrma kikionekana kutoka angani
Kimbunga Irma kimeelekea visiwa vya Turks na Caicos baada ya kusababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean na kuwaua takriban watu 14.
Visiwa vilivyo nyanda za chini vinaripotiwa kuwa kwenye hatari kubwa kukiwa na uwezekano wa kupigwa na mawimbi ya hadi urefu wa mita 6 kuliko viwango vya kawaida.
_97696988_041501441-1Haki miliki ya picha
Image captionMitaa iliyofurika huko St Martin
Kumeripotiwa uharibifu na mafuriko nchini Haiti ambapo miundo mbinu bado ni mibaya tangu litokee tetemeo la ardhi mwaka 2010.Irma ni kimbunga cha kiwango cha tano.
Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi cha kimbunga na upepo wake una kasi ya kilomita 280 kwa saa.
_97710246_mediaitem97710245Haki miliki ya picha
Image captionMafuriko huko St Martin
Takiban watu milioni 1.2 wameathiriwa na kimbunga Irma na idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa haraka hadi watu milioni 26.
Kuna wasi wasi kuwa ugonjwa unaweza kusambaa kwa haraka maeneo ambapo maji ya kunywa na huduma za usafi zimeathirika, na maafisa wameonya kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.
_97692018_martinreutersHaki miliki ya picha
Image captionMafuriko zaidi Saint Martin
Irma sasa kiko karibu na visiwa vya Turks na Caicos na huenda pia kikaelekea huko Bahamas.
Kimbunga hicho kinatarajiwa kufika Cuba baadaye kabla ya kupinga jimbo la Florida huko Marekani mwishoni mwa wiki huku mkuu wa shirika la huduma za dharura la Mareknia akitabiri uharibifu mkubwa.
_97714195_mediaitem97703492Haki miliki ya picha
Image captionUharibifu huko Sint Maarten
Maandalizi ya kuwasili kimbunga Irma yalifanywa katika visiwa vya Turks na Caicos ambayo ni himaya ya Uingereza yenye vyenye watu 35,000.
Irma pia kilisababisha uharibifu kwa paa za nyumba na kawi katik sehemu za kaskazini mwa Jamhuri ya Dominica.
Nchini Cuba maelfu ya watalii kutoka maeneo ya kistarehe ya pwani wamehamishwa.
_97695412_041498349-1Haki miliki ya picha
Image captionBiashara zafungwa Miami kabla ya kimbunga@habari na bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...