MPANDA
Baadhi ya wahanga wa bomoa bomoa mtaa wa
msasani kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wameelezea wasiwasi wa kutopata
viwanja kwa wakati kutokana na zoezi la kupewa viwanja kutoshughulikiwa haraka.
Wakizungumza na Mpanda Radio wakazi hao pamoja
na mambo mengine wamesema kwa kiasi kikubwa suala la kutafuta viwanja ameachiwa
mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda Hotel.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Msasani
Bw.Jonard Makoli amesema zoezi la kupata viwanja linaendelea vizuri ikiwemo
kupata viwanja vingine nje ya eneo la Kampuni na Airtel.
Wakazi zaidi ya 300 wanatakiwa kuondoka katika
eneo linalodaiwa kuwa hifadhi ya reli kabla ya mwezi Januari Mwakani kwa
kuhamia katika maeneo watakayoelekezwa na serikali.
No comments:
Post a Comment